Idara ya Quráni imeandaa semina ya kuhifadhi Quráni na usomani sahihi

Maoni katika picha
Idara ya Quráni chini ya ofisi ya tablighi ya Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeandaa semina ya (uwanja wa uzuri wa Quráni) kuhifadhi na usomaji sahihi.

Kiongozi wa idara bibi Fatuma Sayyid Abbasi Mussawi amesema: “Semina inalenga kunufaika na kipindi cha likizo za majira ya joto (kiangazi) kwa kufundisha usomaji sahihi wa Quráni pamoja na kuhifadhi surat (Luqmaan), sura hiyo imejaa mafundisho ya tabia njema kwa vijana pamoja na mambo mengine”.

Akaongeza kuwa: “Semina itafanywa kwa kutumia mtandao wa Telegram kwa vijana wenye umri wa miaka (12 hadi 15)”.

Kuhusu masharti ya kujiunga na semina, akasema: “Mshiriki hatakiwi kuwa anashiriki semina au masomo sehemu nyingine, pamoja na kuzingatia umri tulio taja na kila mshiriki atume kopi ya kitambulisho cha taifa au nyaraka zozote zinazo mtambulisha, kutakuwa na vyeti vya ushiriki baada ya semina”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: