Atabatu Abbasiyya tukufu inashiriki katika maonyesho ya kimataifa ya vitabu mjini Bagdad

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu inashiriki katika maonyesho ya kimataifa ya vitabu mjini Bagdad awamu ya ishirini na mbili, kupitia kitengo cha habari na utamaduni na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, yanayo anza siku ya Alkhamisi (28 Shawwal 1442h) sawa na tarehe (10 Juni 2021m) chini ya kauli mbiu isemayo (Kitaba na taifa) kwa ushiriki wa zaidi ya taasisi (220) za usambazaji wa vitabu kitaifa na kimataifa kutoka ndani na nje ya nchi yatakayo dumu kwa muda wa siku kumi.

Tumeongea na kiongozi wa idara ya maonyesho Ustadh Muhammad Aáraji amesema kuwa: “Kushiriki kwenye maonyesho haya ni muhimu aidha ni sehemu ya ratiba ya ushiriki wa maonyesho mbalimbali ya kitaifa na kimataifa, yanasaidia kuhamasisha utamaduni wa kusoma na kuandika, pamoja na kutoa nafasi kwa watu wanaotembelea maonyesho, kuangalia harakati mbalimbali zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, ushiriki wa mwaka huu ni muendelezo wa ushiriki wa miaka ya nyuma, tumeshiriki kupitia vitengo viwili ambayo vinamachapisho mbalimbali yanayo husu tabaka zote za watu”.

Akaongeza kuwa: “Ushiriki huu utakuwa muendelezo wa mafanikio yaliyo patikana katika ushiriki uliotangulia kwaidhini ya Mwenyezi Mungu, hakika vitabu na machapisho tuliyo nayo yanaonyesha ukubwa wa kazi za kielimu na kitamaduni zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya, kwenye sekta ya utamaduni, elimu, turathi na zinginezo, aidha ni matokeo halisi ya kazi zinazofanywa na Ataba takatifu, kuanzia uandishi hadi uchapaji, nayo ni sifa ya pekee tuliyo nayo tofauti na taasisi zingine”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imesha shiriki mara nyingi mwenye maonyesho ya kimataifa yanayo fanyika Bagdad, na huzingatia kuwa maonyesho muhimu kwake, pamoja na maonyesho mengine mengi ya kitaifa na kimataifa ambayo hufanywa ndani na nje ya Iraq, yanayo endana na mwenendo wake wa kusambaza utamaduni na elimu ya Ahlulbait (a.s), matawi yake hupata muitikio mkubwa kutoka kwa wananchi, na huhakikisha inakuwa na machapisho mapya katika kila maonyesho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: