Kumbukumbu ya kuolewa kwa Ummul-Banina na kiongozi wa waislamu (a.s)

Maoni katika picha
Kamati ya Nurul-Hessein (a.s) kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya hafla ya wanawake awamu ya pili, la kuadhimisha tukio la kiongozi wa waislamu Ali bun Abu Twalib (a.s) kumuoa bibi mtukufu Ummul-Banina (a.s) inayo sadifu siku ya mwezi tatu Dhulqaadah 1442h sawa na tarehe (13 Juni 2021m) ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Ataba tukufu, na kuhudhuriwa na wakuu wa vitengo na idara pamoja na wakazi wa Karbala na wawakilishi wa mawakibu na vikundi tofauti.

Rais wa kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kongamano hili linafanywa kwa mara ya pili kufuatia kauli ya Imamu Swadiq (a.s) isemayo: (Wafuasi wetu wameumbwa kutokana na udongo wetu, wanafurahi kwa furaha yetu na wanahuzunika kwa huzuni zetu), hivyo kamati huandaa maadhimisho ya tukio hili tukufu, tukio la kiongozi wa waumini kumuoa Ummul-Banina (a.s), nayo ni fursa ya kuongea maisha ya bibi huyu mtukufu na nafasi yake mbele ya Mwenyezi Mungu na Ahlulbait (a.s)”.

Akaongeza kuwa: “Kumkumbuka bibi huyu mtukufu ni kukumbuka msimamo wake na utiifu wake kwa Imamu wa zama zake Ali bun Abu Twalib (a.s), alijitolea watoto wake waene wanaojulikana ushujaa wao katika historia ya kiislamu linapo elezewa tukio la Karbala, hakika alikuwa muaminifu yeye na watoto wake, tangu alipoingia katika nyumba ya Imamu Ali (a.s) hadi kufa kwake (a.s) katika mji wa Madina”.

Kiongozi wa kamati ya Nurul-Hussein (a.s) akasema kuwa: “Kongamano hili linafanywa kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu, ukizingatia kuwa kamati yetu imejikita katika kuadhimisha matukio yanayo husu Ahlulbait (a.s), hivyo tumeandaa ratiba maalum ya kuadhimisha tukio hili tukufu, kongamano limepambwa na mawaidha mbalimbali pamoja na mashairi kuhusu utukufu wa bibi huyu na ushujaa wake, bila kusahau ushujaa wa watoto wake wanne wakiongozwa na Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Kumbuka kuwa vitabu vya historia havijaandika kwa urefu tukio la kiongozi wa waislamu kumuoa Ummul-Banina (a.s), hii ni tarehe ya pili katika tarehe zinazotajwa kufanyika kwa ndoa hiyo, kamati ya Nurul-Hussein (a.s) imechagua kufanya kongamano katika siku hii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: