Mahafali ya Quráni ya kuadhimisha kuzaliwa kwa bibi Maasuma (a.s)

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia tawi lake la wilaya ya Hindiyya mashariki ya mkoa wa Karbala, imefanya hafla ya kuadhimisha kuzaliwa kwa bibi maasumah bint Imamu Mussa bun Jafari (a.s) kwa kuandaa hafla ya usomaji wa Quráni ambayo imeshiriki idadi kubwa ya wasomaji pamoja na wakazi wa mji huo.

Hafla hiyo imefanywa katika malalo ya Sayyid Ahmadi bun Imamu Mussa bun Jafari (a.s), baada ya Quráni ya ufunguzi, ukafuata ujumbe kutoka kwa kiongozi wa tawi Sayyid Haamid Marábi, ametoa pongeza kwa kuadhimisha tukio hili tukufu, halafu akazungumza kuhusu maisha ya bibi Maasumah (a.s), na namna alivyo kuwa na hadhi kubwa kushinda ndugu zake, alikuwa na elimu kubwa tangu akiwa mdogo, alizaliwa na kukulia katika nyumba takatifu, alilelewa na kusoma kwa kaka yake Imamu Ali bun Mussa Ridhwa (a.s), alijulikana kwa kuhifadhi Quráni na kusimulia hadithi tukufu.

Baada ya hapo masikio ya wahudhuriaji yakaburudishwa kwa Quráni tukufu. Kumbuka kuwa tawi hili hufanya harakati mbalimbali za Quráni, pamoja na miradi mingine hapa wilayani inayo lenga kufundisha kitabu cha Mwenyezi Mungu katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: