Ugeni kutoka shirika la chakula na kilimo (Fao) chini ya umoja wa mataifa jioni ya Jumapili, umetembelea shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Khairul-Juud lililo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Ugeni umeongozwa na muwakilishi wa shirika hilo hapa Iraq Dokta Swalahu Haji Hassan, wameangalia uzalishaji wa shirika la Khairul-Juud, na kusikiliza maelezo kutoka kwa wasimamizi wa shirika.
Bwana Hassan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tumefurahi kutembelea shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Khairul-Juud na tumeona bidhaa zake zenye ubora mkubwa”.
Akaongeza kuwa: “Tumejadili kuhusu mazao ya kilimo na bidhaa za viwandani pamoja na vitakasa mikono na barakoa zilizopo sokoni na duniani kwa ujumla”.
Akasema: “Mazungumzo yalijikita katika kuimarisha ushirikiano baina yetu, kutakuwa na mikutano mingine tutakayo fanya kujadili mambo yanayo husiana na kilimo kwa faida, soko la Iraq na kutimiza malengo ya shirika”.