Wanafunzi wa chuo kikuu cha Karbala wamefanya tamasha la kuhitimu masomo katika kumbi za haram za Ataba mbili tukufu

Maoni katika picha
Wanafunzi wa kitivo cha malezi na taaluma katika chuo kikuu cha Karbala, wamefanya tamasha la kuhitimu masomo yao, ndani ya haram tukufu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kufuata utaratibu maalum ulioandaliwa na idara ya mahusiano ya vyuo vikuu na shule, chini ya kitengo cha uhusiano cha Atabatu Abbasiyya.

Tumeongea na kiongozi wa habari Ustadh Mustwafa Kadhwimi kuhusu tamasha hilo, amesema: “Kukaribisha wanafunzi hawa ni sehemu ya harakati za idara, katika mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, tamasha hili limefanyika baada ya kupokea maombi rasmi kutoka kwa mkuu wa chuo”.

Akaongeza kuwa: “Tumeandaa utaratibu kamili wa hawa wanafunzi, wenye vipengele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni: (Kufanya ziara ya vikundi katika malalo mbili takatifu, kutembea ndani ya maeneo ya Ataba mbili takatifu, kupiga picha za ukumbusho ndani ya ukumbi wa haram ya Abbasi (a.s)”.

Akamaliza kwa kusema: “Kufanya tamasha la kuhitimu masomo katika eneo hili takatifu kuna athari nzuri kwa wanafunzi”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imepiga hatua kubwa katika kusaidia vyuo vikuu, inaprogram na miradi mingi katika swala hilo, kuna miradi inayo lenga wakufunzi na mingine inalenga wanafunzi wa vyuo, program ya Multaqa-Thaqafi ni moja ya program nyingi zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: