Kufanyika warsha ya kielimu kuhusu ufundishaji kwa njia ya mtandao

Maoni katika picha
Asubuhi ya Jumanne ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, chini ya usimamizi wa Ataba na chuo cha Twafu pamoja na wawakilishi wa wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu, zilianza shughuli za warsha ya kielimu iliyo pewa jina la (Nafasi ya mawasiliano na mashirika ya simu ganja katika kukuza ufundishaji kwa njia ya mtandao hapa Iraq).

Warsha imehudhuriwa na wawakilishi wa wizara ya (elimu ya juu na utafiti wa kielimu, malezi na mawasiliano), pamoja na marais wa vyuo, wakuu wa vitivo na viongozi wa idara za elimu.

Warsha imefunguliwa kwa Quráni tukufu iliyosomwa na Sayyid Haidari Jaluhani, ikafuatiwa na kisomo cha surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukasikilizwa wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya (Lahnul-Ibaa), ukafuata ujumbe wa Atabatu Abbasiyya ulio wasilishwa na rais wa chuo cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Ataba tukufu, Dokta Muayyad Ghazali, miongoni mwa aliyosema ni: “Katika kila changamoto ambayo taifa letu linapitia, Atabatu Abbasiyya imekuwa ikitafuta njia ya kutatua changamoto hiyo kadri iwezavyo, sawa iwe ya kimaisha au kielimu”.

Akaongeza kuwa: “Dunia ilipopata changamoto ya Korona, sekta ya elimu ikapata vikwazo vingi, Ataba ikaja na mbinu nyingi za kusaidia jamii, idara ya mawasiliano ikaanzisha ujifunzaji kwa njia ya mtandao, taasisi zote za elimu zilizo chini ya Ataba ziliendelea kufundisha kwa kutumia njia hiyo, ikasaidia kuziba pengo katika sekta ya elimu”.

Akamaliza kwa kusema: “Hakika ufundishaji wa njia ya mtandao ni vizuri ukajadiliwa na kila upande kwa ajili ya kuangalia maendeleo yake, ndipo taasisi za Ataba tukufu chini ya chuo kikuu cha Al-Ameed, Alkafeel na kituo cha Alkafeel cha taaluma pamoja na wadau wengine tumeshirikiana kuandaa warsha hii”.

Ukafuata ujumbe wa wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu uliowasilishwa na muwakilishi wa wizara ya elimu kitengo cha taaluma za mitandao uliowasilishwa na Dokta Aamir Salim Amiir, akaishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kufanya warsha hii muhimu, chini ya usimamizi wa vyuo vyake vikuu vya Al-Ameed na Alkafeel.

Kisha ukafuata ujumbe wa wizara ya mawasiliano ulio wasilishwa na Ustadh Naadhim Laftah, akaeleza kazi zinazo fanywa na wizara katika kusaidia usomaji kwa njia ya mtandao hapa nchini, na mikakati ya kuboresha usomaji huo, sambamba na kuishukuru Atabatu Abbasiyya kwa kazi kubwa inayo fanya katika sekta ya ufundishaji kwa njia ya mtandao.

Ukafuata ujumbe wa chuo cha Twafu uliowasilishwa na mkuu wa chuo Dokta Karim Mazáli, akasema: “Kupitia warsha hii tunatarajia tuweze kutatua changamoto zilizopo katika sekta ya usomaji kwa njia ya mtandao, na kupata ufumbuzi wa vikwazo mbalimbali, shukrani za pekee ziende kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kutupa nafasi katika warsha hii, na hili sio geni kwao, huu ni muendelezo wa kazi nyingi na kubwa zinazo fanywa na Ataba katika kila sekta hasa upande wa elimu na malezi”.

Baada ya hapo shughuli za uwasilishaji wa mada za kitafiti ikaanza chini ya usimamizi wa Dokta Najmu Ambdallah makamo rais wa chuo kikuu cha Karbala, jumla ya mada tano zikawasilishwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: