Sauti za usomaji wa Quráni tukufu zasikika ndani ya haram ya Maqaam ya mshirika wake

Maoni katika picha
Maqaam ya Imamu Mahadi (a.s) katika mji wa Karbala asubuhi ya Ijumaa, imefanya kikao cha usomaji wa Quráni, iliyo andaliwa na kusimamiwa na kitengo cha miradi ya Quráni kilicho chini ya Maahadi ya Quráni tukufu katika Atabatu Abbasiyya, wasomaji wa Maahadi wameshiriki kwenye usomaji huo pamoja na wageni, aidha kisomo hiki ni sehemu ya kuonyesha utukufu wa Quráni na umuhimu wake katika jamii.

Maahadi imealika wanafunzi wa wasomo ya Dini wanaoshiriki kwenye semina ya kuandaa walimu wa Quráni, inayo endeshwa chini ya ratiba ya miradi ya Quráni na kusimamiwa na tawi la Maahadi ya Quráni katika mkoa wa Najafu tukufu, wamepata utukufu wa kushiriki katika usomaji huo na kusikiliza Quráni tukufu.

Walioshiriki katika usomaji ni Shekh Qudaamah Mundhir, Muhammad Ridhwa Salmaan, Ahmadi Zaamiliy, Muhammad Ali Rashidi, mazuwaru wa Maqaam hiyo takatifu pia wamehudhuria katika kikao hicho cha usomaji wa Quráni.

Kumbuka kuwa kituo cha miradi ya Quráni kinafanya vikao vya usomaji wa Quráni kila wiki kuanzia saa kumi na moja kila siku ya Alkhamisi ndani ya Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f), na hualika wasomaji wa Quráni tukufu wa hapa nchini, vikao hivyo vya usomaji wa Quráni hurushwa mubashara kwenye chanel ya Quráni ambayo ipo chini ya kituo cha luninga za Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: