Kamati ya maelekezo na msaada yatembelea vikosi vya Swalahu-Dini

Maoni katika picha
Kamati ya maelekezo na msaada chini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetembelea vikosi vya mkoa wa Swalahu-Dini, kimekutana na wapiganaji wa mkoa huo na kuwapa zawadi kutoka katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Rais wa kamati hiyo Shekh Haidari Aridhwi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ziara imehusisha kutembelea vikosi vya Swalahu-Dini, Samaraa, Liwaau/22, kikosi cha tatu cha Liwaau/313 pamoja na Liwaau ya saba kikosi cha wapiganaji wa Nahariyya, na kuwahimiza washikamane na maelekezo ya kuchukua tahadhari dhidi ya njama za maadui, aidha tumefikisha salamu na dua za ndugu zao watumishi wa Atabatu Abbasiyya na viongozi wao, sambamba na kuwapa zawadi za kutabaruku na malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Wapiganaji wameipongeza Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kuwa pamoja nao wakati wote katika uwanja wa vita na kwenye maeneo yaliyokombolewa, wakasisitiza kuwa jambo hilo linawatia moyo na kuwajengea ujasiri wakuendelea kuwa ngome madhubuti kwa kila atakaetaka kuchezea amani na utulivu wa taifa hili.

Kumbuka kuwa kamati ya maelekezo na msaada ikochini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imesimama imara kusaidia wapiganaji wa Hashdu-Shaábi katika vikosi tofauti, chini ya ratiba maalum sawa sawa uwe wakati wa vita au baada yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: