Semina ya wasichana kuhusu misingi ya uokozi wa awali

Kwa kushirikiana na idara ya shule za Dini za Alkafeel kitengo cha wasichana, idara ya Swidiiqah Twahirah (a.s) ofisi ya madaktari inaendesha semina za utoaji wa huduma ya kwanza na jinsi ya kupambana na majanga, kwa watumishi wa kujitolea kutoka Karbala na mikoani, kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kufanya huduma za uokozi, ili waweze kutoa huduma bora kwa mazuwaru, hususan katika ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu.

Kiongozi wa Irara bibi Bushra Kinani ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Semina hii ni sehemu ya utaratibu maalum uliopangwa kwa watumishi wa kujitolea zinahusu sekta ya (Udaktari – Uuguzi na Famasia) pamoja na fani zingine, wakufunzi wametoka idara ya afya ya mkoa wa Karbala na hospitali ya Alkafeel, chini ya usimamizi wa idara ya madaktari wa Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaongeza kuwa: “Tumeandaa ratiba maalum ya utoaji wa semina hii kwa watu wanaojitolea kutoka kila mkoa, kwa muda wa saa nne kila simu, kila semina wanafundishwa kwa nadhariyya na vitendo, ndani ya ukumbi wa kituo cha Swidiiqah Twahirah wa harakati za wasichana pamoja na hospitali ya Alkafeel”.

Akafafanua kuwa: “Wanafundishwa vitu vingi, miongoni mwa vitu hivyo ni:

  • - Maandalizi ya utoaji wa huduma ya kwanza.
  • - Aina za majanga na namna ya kupambana nayo.
  • - Misingi ya utoaji wa huduma ya kwanza.
  • - Njia za kuzuwia kutiririka damu na mambo ya kufanya.
  • - Kanuni za kuokoa na kubeba majeruhi.
  • - Masharti ya uokozi.
  • - Vipaombele vya uokozi.
  • - Njia muhimu za utoaji wa huduma ya kwanza.
  • - Uokozi wa mtu mwenye matatizo ya moyo.
  • - Uokozi wa mtu asiejitambua”.

Akamaliza kwa kusema: Baada ya kumaliza semina hii tunatarajia kuanzisha kikosi cha waokozi wa kike, wenye uwezo wa kupambana na janga lolote linaloweza kutokea (Allah atuepushie).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: