Wanafunzi wa chuo cha Albayaan wapo katika ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Idara ya mahusiano ya vyuo na shule chini ya kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya imepokea wanafunzi wa kitivo cha uuguzi kutoka chuo kikuu cha Albayaan, chini ya utaratibu wake maalum wa kupokea ugeni wa wanafunzi kutoka vyuoni na mashuleni, kwa ajili ya kudumisha mawasiliano na kundi hilo muhimu, kwani wao ndio wajenzi wa Iraq ijayo, na kushirikiana nao katika furaha ya kuhitimu masomo.

Mwenyeji wa ugeni huo na msimamizi wa ratiba Ustadh Haidari Maámaar ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kupokea ugeni wa wanafunzi hususan wa chuo ni moja ya harakati za idara yetu, iliyopo katika mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel”.

Akaongeza kuwa: “Hupokea ugeni wa wanafunzi baada ya kupata maombi kutoka kwa mkuu wa chuo, wanaratiba kamili yenye vipengele vingi, ilianza kwa kupokea na kuwatambulisha harakati za idara kwa ujumla pamoja na mradi wake uitwao (kijana wa Alkafeel), kisha wakafanya ibada ya ziara na kusoma dua kwa pamoja ndani ya ukumbi wa Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaendelea kusema: “Kisha ugeni ukaelekea katika malalo ya Abu Abdillahi Hussein (a.s), baada ya kuwasiliana na uongozi wa Atabatu Husseiniyya, wakaenda kufanya ziara ya pamoja iliyo ongozwa na mmoja wa masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Husseiniyya, wakahitimisha na kula chakula cha baraka katika mgahawa (mudhifu) wa Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na kupiga picha za ukumbusho ndani ya malalo zote mbili takatifu, kisha wageni wakaagwa kwa maneno mazuri na kuwaombea dua ya kupata mafanikio katika maisha yao ya kielimu, ziara hii iwe ni msingi wa mabadiliko katika maisha yao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: