Shule za Al-Ameed zinafanya maonyesho ya kazi za mikono

Maoni katika picha
Shule ya upili (sekondari) Alqamaru ya wasichana ambayo ipo chini ya shule za Al-Ameed imefanya maonyesho ya kazi za mikono chini ya kauli mbiu isemayo: (Fani ya uchoraji miongoni mwa maumbo ya tiba), yamehusisha picha za kuchora kwa mikono na mabango yaliyo andikwa hati za kiarabu, zilizo andikwa kwa mikono na wanafunzi wa shule.

Kiongozi wa dawati la malezi na hati za kiarabu katika shule za Al-Ameed, Ustadh Abdulkarim Shimri ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Shule za Al-Ameed zinaendelea kufanya harakati mbalimbali, kwa lengo la kuwajengea uwezo wanafunzi wenye vipaji tofauti, sambamba na kuzingatia tofauti zao kimasomo, Atabatu Abbasiyya tukufu inazipa kipaombele zaidi kazi za mikono, imekuwa ikiandaa maonyesho mengi ya kazi hizo, likiwemo onyesho hili”.

Akaongeza kuwa: “Maonyesho haya ni sehemu ya ratiba maalum ya shule za Al-Ameed, aidha ni kielelezo cha kuonyesha namna tunavyo jali kazi za mikono”, akasisitiza kuwa: “Wakati wa maambukizi ya virusi vya Korona vilivyo athiri sekta nyingi za maisha, shule za Al-Ameed zimeendelea kufanya maonyesho pamoja na wanafunzi waliopo shuleni, na kukamilisha maandalizi ya maonyesho hayo”.

Watu walioshiriki katika ufunguzi wa maonyesho haya, wamefurahishwa na kazi mbalimbali zinazo onyeshwa, zinaeleza kazi kubwa inayofanywa na shule, katika kukuza vipaji vya wanafunzi, uongozi wa kitengo cha malezi umempa zawadi mwalimu wa Sanaa kutokana na kazi kubwa aliyofanya ya kuandaa maonyesho haya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: