Mradi wa Quráni kwa wanafunzi wa Dini umepokea wageni kutoka hauza ya kielimu

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Najafu imepokea ugeni wa walimu na viongozi wa hauza, katika mradi wa Quráni wa wanafunzi wa Dini unaofanywa na tawi kwa mwaka wa tano mfululizo.

Maahadi imempokea Mheshimiwa Sayyid Muhammad Swadiq Khurasani, Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Ashukuri na Mheshimiwa Sayyid Muhammad Ali Bahrul-Uluum.

Viongozi hao wamekutana na washiriki wa semina ya kuandaa walimu wa Quráni tukufu, wakafafanua mada mbalimbali za Quráni takatifu, wakasisitiza ulazima wa kushikamana na vizito viwili na kuvitumikia.

Aidha wamebainisha utukufu wa kujifunza Quráni na kwenda kuifundisha katika jamii, wakapongeza kazi inayofanywa na Maahadi ya Quráni tukufu ya kuendesha program mbalimbali za Quráni.

Kumbuka kuwa kupokea ugeni huo ni sehemu ya ratiba maalum ya kuwakutanisha wanafunzi wa semina na viongozi wa dini pamoja na walimu wa hauza ya Najafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: