Multaqal-Qamaru yakaribisha kundi la wanafunzi wa elimu ya juu

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni Multaqal-Qamaru chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimepokea kundi la wanafunzi wa elimu ya juu (dokta) kutoka chuo kikuu cha Baabil wanaosomea fani tofauti, chini ya ratiba maalum ya kundi hili inayo lenga kudumisha mawasiliano.

Mkuu wa kituo Shekh Haarith Dahi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ratiba iliyoandaliwa kwa ajili ya makundi ya kijamii inavipengele vingi, kunasehemu inayohusu vyuo vikuu, ukizingatia kuwa kundi hilo linakubalika katika jamii kwa ujumla”.

Akaongeza kuwa: “Baada ya kupokea kundi hilo tukufu na kukamilisha ibada ya ziara na dua, tumekutana nao katika ukumbi wa Qassim (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya, tumewaeleza kuhusu harakati zinazo fanywa na kituo pamoja na Atabatu Abbasiyya kwa ujumla, hususan miradi inayochangia kumjenga mwanaadamu kielimu na kitamaduni, pamoja na kumuwezesha kupambana na changamoto za kijamii”.

Akaendelea kusema: “Baada ya hapo walipewa mawaidha yanayo husu malezi na jamii ya kidini, kwa kulinganisha na mazingira tunayoishi kwa sasa, halafu kukawa na mjadala kuhusu mada iliyo wasilishwa, pamoja na kusikiliza maoni na mapendekezo kuhusu shughuli zinazo fanywa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: