Atabatu Abbasiyya tukufu inagawa maji safi kwa vijiji vinne

Maoni katika picha
Watumishi wa idara ya maji chini ya kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wamejenga kituo cha maji (R.O station) katika kijiji cha Baidhwah mkoani Muthanna, kwa lengo la kugawa maji kwa wakazi wa kijiji hicho na vijiji vingine vitatu na kuwapunguzia shida ya maji wakazi wa vijiji hivyo.

Kiongozi wa idara ya maji Mhandisi Basam Hashimiy ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ujenzi wa kituo hiki umefanywa baada ya kuletwa maombi katika Atabatu Abbasiyya na wakazi wa vijiji hivi, wakieleza shida kubwa ya maji safi ya kunywa waliyo nayo, wamejibiwa haraka na idara yetu kuamrishwa kuja kujenga kituo hiki”.

Akaongeza kuwa: “Kituo kimejengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa (mita 180) kinauwezo wa kuzalisha maji (RO) lita 48 elfu kwa siku, kiwango ambacho kinatosha kwa wakazi wote wa vijiji hivyo wapatao (900) takriban, kutoka nyumba (1500)”.

Akabainisha kuwa: “Vifaa vyote vilivyo tumika katika ujenzi wa kituo hiki vinaubora wa kimataifa na uwezo mkubwa, chanzo cha maji ya kituo hiki ni maji ya mto ambayo yanasafishwa na kutunzwa vizuri kisha yanasambazwa kwa matumizi”.

Akafafanua kuwa: “Kituo kimejengewa paa na kuwekwa zege sakafu yake pamoja na kuwekwa njia mbalimbali za maji”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu inamiradi mingi ya kuhudumia wananchi, miongoni mwa miradi hiyo ipo inayogusa wananchi moja kwa moja, na inafanya kila iwezalo kupunguza shida za wananchi, changamoto kubwa ambayo tumekua mstari wa mbele kuitatua ni tatizo la ukosefu wa maji safi na salama, tumejenga vituo vingi vya maji (R.O station) kwenye maeneo tofauti, watu wengi wamenufaika na vituo hivyo, kuna vituo maalum vilivyojengwa kwa ajili ya kuhudumia mazuwaru na mawakibu ndani na nje ya mkoa wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: