Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu imehitimisha mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa Dini

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Najafu, imefanya hafla ya kuhitimisha mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa Dini walio hitimu awamu ya nne na tano za mradi huo.

Hafla imefanywa ndani ya ukumbi wa jengo la kituo cha kiislamu na masomo ya kimkakati katika mji wa Najafu, imefunguliwa kwa Qur’ani iliyosomwa na Sayyid Taisiri Mussawi, halafu ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq.

Baada ya hapo likafuata neno la ukaribisho lililotolewa na rais wa kituo cha elimu na Qur’ani tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Ahmadi Shekh Ali, miongoni mwa aliyosema ni: “Karibuni sana kwa kuja kushiriki kwenye hafla ya kuhitimu wanafunzi wa mradi huu, waliofundishwa masomo ya Fiqhi na masomo ya Qur’ani pamoja na kuhifadhi Qur’ani, hakika wameona uzuri wa masomo hayo na jinsi yanavyo fungamana”.

Shekh Ali akaongeza kuwa: “Msaada wa kufanya mradi huu katika mwaka wa kwanza ulitoka kwa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Muhammad Hakiim, hatuna budi kutoa shukrani za dhani na pongezi kubwa kwake”.

Hafla ilihusisha filamu fupi iliyo onyesha hatua za mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa Dini, pamoja na maombolezo ya Shekh Abdillahi Dujaili.

Hafla ikahitimishwa kwa kuwapa zawadi wanafunzi walio hitimu na kufanya vizuri kwenye mradi huu, pamoja na viongozi wa hauza na walimu wa sekula.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: