Atabatu Abbasiyya tukufu inakarabati moja ya shule za Karbala

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya, wameanza kukarabati shule ya Abbasiyya, moja ya shule zilizopo katika mkoa wa Karbala, iliyokua inahitaji ukarabati katika maeneo mengi muhimu, kazi hii ni sehemu ya ratiba ya kusaidia sekta ya elimu na kuweka mazingira mazuri kwa wanafunzi, kwa kukarabati shule zilizo telekezwa.

Msimamizi wa kazi hii Ustadh Hassan Abdulhussein ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Baada ya kupokea maombi kutoka kwa wakazi wa kitengoji hicho na wazazi wa wanafunzi wanaosoma kwenye shule hiyo pamoja na uongozi wa shule, Ataba uliunda kikosi kazi cha mafundi kwa ajili ya kubaini mapungufu yaliyopo katika shule hiyo na aina ya matengenezo yanayo hitajika, kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri ya usomaji wa wanafunzi”.

Akaongeza kuwa: “Kazi inaendelea kama ilivyo pangwa, inahusisha kujenga (kuweka ruva) njia za shule zenye urefu wa mita (300) pamoja na kuweka marumaru madarasani ambapo yanakadiriwa kuwa na ukubwa wa mita (500), kazi hiyo inatanguliwa na kutoa vifaa vya zamani na kusawazisha ardhi”.

Akabainisha kuwa: “Sambamba na kupaka rangi kuta za shule zenye urefu wa mita (600) baada ya kuzikarabati, kuzisawazisha na kuondoa rangi ya zamani iliyokuwa imechakaa, hali kadhalika tumesawazisha uwanja wa shule wenye ukubwa wa mita (250) ambayo ni sehemu pekee ya kuchezea wanafunzi”.

Kumbuka kuwa kazi hii ni sehemu ya miradi ya kibinaadamu inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kukarabati baadhi ya majengo ya serikali yaliyopo katika hali mbaya, imesha karabati majengo mengi ya shule na taasisi za kibinaadamu pamboja na hospitali mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: