Kuanza maandalizi ya awamu ya nne ya kongamano la makumbusho ya Alkafeel kimataifa

Maoni katika picha
Kamati mbili ya maandalizi na elimu zimeanza kufanya maandalizi ya kongamano la makumbusho ya Alkafeel kimataifa, litakalo fanyika kwa mara ya nne mwaka kesho, kamati hizo zimekutana kuandaa mpango wa pamoja wa kongamano hilo.

Tumeongea na rais wa kitengo cha makumbusho ya Alkafeel Ustadh Swadiq Laazim, amesema kuwa: “Kongamano la makumbusho ya Alkafeel kimataifa huandaliwa na kusimamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, awamu zilizo tangulia zilikua na mafanikio makubwa na zilipata muitikio mzuri”.

Akaongeza kuwa: “Kikao hicho kimehudhuriwa na wawakilishi wa chou kikuu cha Bagdad/ kitivo cha Adabu/ kitengo cha athari na turathi, na chou kikuu cha Baabil/ kitivo cha Adabu/ kitengo cha athari na turathi, na chou kikuu cha Kufa/ kitivo cha athari na turathi, wamejadili mada zitakazo wasilishwa kwenye kongamano, pamoja na kuchagua anuani ya kongamano, na wameweka maazimio yatakayo jadiliwa katika kikao kijacho”.

Kumbuka kuwa kongamano linalenga mambo yafuatayo:

  • - Wito wa kutunza turathi, mazingira na utamaduni.
  • - Kusaidia taasisi za Dini na kiraia kuanzisha makumbusho na kukuza fani ya makumbusho.
  • - Kujenga ushirikiano na taasisi za makumbusho za kitaifa na kimataifa.
  • - Kuongeza uwezo wa utendaji katika idara za makumbusho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: