Msiba wa Imamu Baaqir (a.s) umetanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Mazingira ya huzuni yametanda katika jengo la Atabatu Abbasiyya tukufu, kufuatia kuomboleza kifo cha Imamu Muhammad Albaaqir (a.s), aliyekufa mwezi saba Dhulhijjah.

Kuta za Ataba tukufu zimewekwa mapambo meusi yaliyo andikwa maneno yanayo ashiria huzuni na machungu katika nyoyo za wafuasi wa Ahlulbait (a.s).

Kama kawaida katika kumbukumbu za vifo vya watu wa nyumba ya Mtume (a.s), Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba ya uombolezaji yenye vipengele vingi, ikiwa ni pamoja na kufanya majlisi ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuandaa kupokea waombolezaji na mawakibu.

Kumbuka kuwa Imamu Baaqir (a.s) alizaliwa mwezi wa Rajabu mwaka wa (57) hijiriyya katika mji wa Madina, akafa mwezi (7 Dhulhijjah 114h) kwa sumu aliyopewa na Ibrahim bun Walidi bun Hisham bun Abdulmaliki wakati wa utawali wake, akazikwa (a.s) katika makaburi ya Baqii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: