Shindano la (Baina Swafa na Marwa) la wasichana

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya kinaendesha shindano lenye anuani isemayo (Baina Swafa na Marwa) kwa wasichana wenye umri wa miaka (13 – 18) kutokana na kukaribia sikukuu ya Idul-Adh-ha, na kutoa wito kwa kila anayependa kushiriki aingie kupitia mtandao.

Kiongozi wa kituo bibi Asmahani Ibrahim ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hili ni moja ya mashindano mengi yanayo simamiwa na kituo, ambayo hufanywa kutokana na matukio, kwa lengo la kutoa elimu na kukomaza akili za kundi lengwa”.

Akabainisha kuwa: “Washiriki wa shindano hili wataweza kutuma majibu yao katika siku zote za Idul-Adh-ha, kisha majibu sahihi yatapigiwa kura, kuna zawadi maalum za washindi zimeandaliwa pamoja na vyeti vya ushiriki kwa wote watakao shiriki, matokeo yatatangazwa kwenye mtandao wa kituo na washindi watapigiwa simu baada ya sikukuu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: