Atabatu Abbasiyya inafanya majlisi za wanawake za kuomboleza kifo cha Imamu Baaqir na balozi wa babu yake Hussein (a.s)

Maoni katika picha
Katika kuomboleza kifo cha Imamu Baaqir na Muslim bun Aqiil balozi wa babu yake Imamu Hussein (a.s), Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara ya wahadhiri wa Husseiniyya imefanya majlisi ya kuomboleza, ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa mihadhara miwili asubuhi na jioni kwa muda wa siku tatu, kuanzia siku ya mwezi sita Dhulhijjah.

Kiongozi wa idara Shekh Abdu Swahibu Twaaiy ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Majlisi hii hufanywa kila mwaka chini ya mradi wa Ummul-Banina (a.s), unaohusika na kuhuisha matukio ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s) likiwemo tukio hili la kifo cha Imamu Baaqir (a.s), na kifo cha balozi wa harakati ya Husseiniyya Muslim bun Aqiil (a.s) aliyekufa tarehe tisa mwezi huu”.

Akaongeza kuwa: “Majlisi ya asubuhi inahutubiwa na Shekhe Mahmuud Sharifi, na jioni inafanywa baada ya Ishaa na kuhutubiwa na Shekhe Haidari Mula kutoka Lebanon, na hufuatiwa na matam ambayo huongozwa na muimbaji Muhammad Hajiraat”.

Akafafanua kuwa: “Kila kinacho fanywa katika ratiba hii ya kuomboleza kinaangazia historia ya watukufu hao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: