Muhimu: Ziara ya siku ya Arafa na Idi kwa niaba ya kila atakaeshindwa kuja kufanya ziara

Maoni katika picha
Mtandao wa kimataifa Alkafeel unatoa wito kwa wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wote, mashariki na magharibi ya dunia, walio mbali na watakao shindwa kuja katika ardhi ya kujitolea (Karbala) kufanya ziara ya siku ya Arafa na Idi kutokana na ugumu wa mazingira ya sasa ya maambukizi ya virusi vya Korona, wasajili majina yao katika ukurasa wa ziara kwaniaba ufuatao: https://alkafeel.net/zyara/.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara ya ufundi chini ya kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya Ustadh Haidari Twalibu Abdul-Amiir amesema: “Mtandao wa Alkafeel hutoa huduma ya ziara kwaniaba, katika siku zenye ziara maalum kama vile ziara ya Arafa na Idi, tunaipa umuhimu mkubwa katika kipindi hiki, kutokana na idadi kubwa ya watu wa ndani na nje ya Iraq kushindwa kuja kutokana na hali ya afya iliyopo”.

Akabainisha kuwa: “Ibada ya ziara itafanywa ndani ya haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika usiku na mchana wa Arafa, pamoja na kusoma dua ya Imamu Hussein (a.s) na swala ya ziara sambamba na ibada zingine na kuwaombea dua watu wote waliojisajili”.

Akafafanua kuwa: “Tumefungua mlango wa usajili mapema katika ukurasa wa ziara kwa niaba, ili kutoa nafasi kwa watu wengi zaidi wajisajili kupitia mitandao yote ya Ataba, pamoja na mitandao ya mawasiliano ya kijamii iliyo chini yetu, masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya watafanya ziara kwa niaba ya kila atakaejisajili”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: