Kumbukumbu ya kifo cha Muslim bun Aqiil katika haram ya mtoto wa Ammi yake (a.s)

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya kifo cha balozi wa Imamu Hussein na mtoto wa Ammi yake Muslim bun Aqiil (a.s), kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya kinafanya majlisi ya kuomboleza, ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuhudhuriwa na mazuwaru pamoja na watumishi wa Ataba.

Majlisi ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu, kisha Shekh Majidi Sultwani kutoka kitengo cha Dini akaongea kuhusu utukufu wa Muslim bun Aqiil na nafasi yake mbele ya Hussein (a.s), na kwa nini Imamu Hussein (a.s) alimteua yeye kwenda katika mji wa Kufa na sio mwingine, akamfanya kuwa balozi wake, aidha Shekh Sultwani ameeleza tukio la kuuwawa Muslim bun Aqiil (a.s).

Kumbuka kuwa siku ya mwezi (9) Dhulhijjah ni siku ya kukumbuka kifo cha balozi wa harakati ya Imamu Hussein Muslim bun Aqiil (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: