Kikosi cha wizara ya elimu kinafuatilia ufanyaji wa mitihani katika chuo kikuu cha Alkafeel

Maoni katika picha
Kikosi cha wizara kinacho husima na masomo kwa njia ya mtandao chini ya wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu, kinaangalia ufanyaji wa mitihani katika chuo kikuu cha Alkafeel, baada ya ziara waliyofanya wakiwa pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Atabatu Abbasiyya tukufu na rais wa kamati ya malezi na elimu ya juu Dokta Abbasi Mussawi, na rais wa chuo Dokta Nuris Muhammad Shahidi Dahani pamoja na wasaidizi wake.

Wameangalia ufanyaji wa mitihani na kukagua kumbi za kufanyia mitihani.

Rais wa chuo amewaambia wajumbe kutoka wizarani kuwa: “Mitihani inaendelea vizuri, tunafuatilia kwa karibu mwenendo wa mitihani kwenye vitivo vyote, kwa ajili ya kuondoa changamoto yote inayoweza kutokea kwa wanafunzi, sambamba na kuandaa vitu vyote vinavyo hitajika katika mitihani kama ilivyo elekezwa na wizara, na kuheshimu masharti ya kujikinga na maambukizi kama yalivyo tajwa na wizara ya afya”.

Baada ya ziara wajumbe kutoka wizarani wamesifu kazi kubwa inayofanywa na chuo kikuu ya ufundishaji na kufanikisha ufanyaji wa mitihani na kuwatakia mafanikio mema.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: