Kufungua mlango wa usajili wa program ya kujenga uwezo

Maoni katika picha
Jumuiya wa Skaut ya Alkafeel chini ya idara ya watoto na makuzi katika kitengo cha Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kufungua mlango wa usajili katika program ya kujenga uwezo kwa kutumia njia ya mtandao awamu ya pili na ya tano, zitakazo husisha mambo mbalimbali ya kielimu, kitamaduni na kisanii, pamoja na mashindano ya kielimu na kitamaduni.

Walengwa ni vijana wenye umri wa miaka (9 – 12) na (13 – 18), miongoni mwa watakayo fundishwa ni:

  • 1- Fani ya picha.
  • 2- Fani ya kuongea.
  • 3- Masomo ya uigizaji.
  • 4- Masomo ya uimbaji.
  • 5- Warsha ya kusimamia mabadiliko.
  • 6- Warsha ya uongozi.
  • 7- Warsha ya miradi midogo.
  • 8- Warsha ya Aqaaid.
  • 9- Warsha ya visa vya Qur’ani.
  • 10- Warsha ya michezo.

Kwa maelezo zaidi unaweza kupiga simu kwa moja ya namba zifuatazo:

Uongozi wa chuo: 07724892039/ 07602326690.

Uongozi wa program: 07830772730/ 07717263946.

Kumbuka kuwa program ya kujenga uwezo huwa na vipengele vingi vya kidini kielimu na kimakuzi, na hulenga kutumia vizuri muda wa vijana kwa kufanya mambo yenye manufaa kwao, aidha hupewa mitihani mbalimbali inayosaidia kuwajenga na kuongeza uwezo wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: