Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu inahitimisha (sehemu ya kwanza) ya semina ya kusimama na kuanza katika usomaji wa Qur’ani

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tawi la Najafu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imehitimisha semina ya kusimama na kuanza katika usomaji wa Qur’ani tukufu.

Semina ilikua na zaidi ya mada ishirini zilizo fundishwa kwa muda wa miezi minne na Dokta Karim Jabri Zubaidi.

Semina hii ni sehemu ya (vikao vya usomaji bora) vinavyo fanywa na Maahadi katika mji wa Najafu na kushiriki makumi ya wanafunzi, sehemu ya pili itaanza siku zijazo.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Najafu hufanya semina mbalimbali za Qur’ani pamoja na harakati tofauti zinazo lenga kufanyiwa kazi mafundisho ya vizito viwili katika jamii.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya kupitia matawi yake tofauti, hufanya program mbalimbali za Qur’ani ndani na nje ya mkoa wa Karbala, pamoja na miradi endelevu ya Qur’ani kwa lengo la kueneza utamaduni wa kusoma Qur’ani katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: