Kunfungua mlango wa ushiriki katika semina ya Skaut

Maoni katika picha
Chini ya kauli mbiu isemayo: (nipe mkate na igizo nitakupa kijana mwenye maadili), kuanzia katika semina ya uigizaji na uendelezaji wa jamii na mataifa, ni moja ya jukwaa la adabu na tamaduni tofauti, jumiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya imefungua mlango wa kushiriki kwenye semina ya kuandaa mwanaskaut muigizaji, ambayo ni sehemu ya tano ya kuendeleza vijana wenye umri wa miaka (13 – 18).

Jumiya imetoa wito kwa kila mwenye sifa na anaependa kushiriki kwenye semina hii ya kujenga uwezo wa wanaskaut ajiunge kupitia link ya telegram ifuatayo @maliiry.

Semina itaanza tarehe (27 Julai 2021m) itakua na mihadhara tofauti ya kujenga uwezo wa washiriki kulingana na vipaji vyao, wakufunzi ni walimu waliobobea katika sekta hiyo, miongoni mwa mada zitakazo fundishwa ni:

  • - Maadili na taratibu za uigizaji.
  • - Mfano wa igizo na muigizaji.
  • - Vifaa vya uigizaji.
  • - Aina za maigizo.
  • - Sauti na uongeaji.

Semina itahusisha masomo ya akhlaq, Aqida na masomo ya kifikra, wale watakao fanya vizuri katika mitihani ya kumaliza semina watapewa vyeti vya ushiriki pamoja na zawadi.

Washiriki wanapata mihadhara ya semina wakati wote na mahala popote, watapewa link maalum wakati wa semina, pamoja na kazi za nyumbani na majaribio, watakao fanya vizuri kwenye semina hii watapewa nafasi ya kushiriki semina ijayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: