Wito wa kushiriki katika semina ya uimbaji

Maoni katika picha
Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya idara ya watoto na makuzi katika kitengo cha habari cha Atabatu Abbasiyya tukufu, imetoa wito wa kushiriki kwenye semina ya uimbaji itakayo fanywa kwa njia ya mtandao kwa wavulana wenye umri wa miaka (10 – 18), ambayo ni sehemu ya mradi wa kujenga uwezo awamu ya tano, kupitia mtandao wa telegram kwa link ifuatayo @maliiry.

Semina itaanza tarehe (27 Julai 2021m) inalenga kuimarisha uwezo wa uimbaji kwa wavulana na kuibua vipaji vyao chini ya wabobezi wa mambo hayo.

Mambo makuu yatakayo fundishwa katika semina hiyo ni:

  • - Historia ya uimbaji.
  • - Adabu za uimbaji.
  • - Maqamaat (mahadhi).

Washiriki wa semina hii watapewa vyeti vya ushiriki baada ya mitihani ya mwisho, pamoja na kugawa zawadi kwa watakao fanya vizuri, mshiriki atapata mada wakati wote sehemu yeyote atakapo kua, watapewa link maalum wakati wa semina, sambamba na kazi pamoja na mitihani, watakao fanya vizuri katika semina hii watapewa nafasi ya kushiriki semina inayo fuata.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: