Kuanza mitihani ya mwisho katika chou kikuu cha Alkafeel chini ya utekelezaji mkali wa masharti ya afya

Maoni katika picha
Jumapili asubuhi mitihani ya mwisho wa mwaka wa masomo (2020 – 2021) imeanza katika chou kikuu cha Alkafeel, chou hicho kimekua mfano wa vyuo vingine vya Iraq kwa kufuata maelekezo ya wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu, na kutii masharti ya kujikinga na maambukizi ya Korona yaliyotolewa na wizara ya afya.

Rais wa chou Dokta Nuris Dahani ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kutokana na maelekezo ya wizara ya elimu ya juu, tumeanza kufanya mitihani ya mwisho kwa wanafunzi kuhudhuria moja kwa moja kwenye vyumba vya mitihani na kwa njia ya mtandao, katika vitivo vyote vya chuo kikuu cha Alkafeel, baada ya kukamilisha maandalizi yote ya kujikinga na maambukizi”.

Akasema: “Tumeweka utaratimu maalum na kanuni za kujikinga na maambukizi, sambamba na kuandaa kumbi zote, na kupunguza wingi wa wanafunzi pamoja na kufuata masharti yote ya kujikinga na maambukizi, kwa ajili ya kulinda usalama wa wanafunzi na wasimamizi wa mitihani”.

Akaongeza kuwa: “Tumezingatia umbali kati ya mtu na mtu katika ukaaji ndani ya vyumba vya mitihani, kanuni na maelekezo yametolewa kwa njia ya mtandao ili kuepusha msongamano, wanafunzi wote wanapimwa afya zao na kupewa barakoa wakati wanapoingia kwenye vyumba vya mitihani, aidha wanaendelea kupewa maelekezo ya chou kila siku, wasimamizi wa mitihani wanafuatilia utekelezaji wa kanuni na taratibu za kujikinga na maambukizi chini ya usimamizi wa rais wa chou”.

Akasisitiza kuwa: “Wanafunzi wote wanafuata kikamilifu taratibu za kujikinga na maambukizi kwa ajili ya kulinda usalama wao”. Akasema: “Ni muhimu wanafunzi kufika mapema kwa ajili ya kuwakagua na kuwapa barakoa sambamba na kuingia kwa kutumia mlango wenye mtambo wa kupuliza dawa”.

Akaongea kuwa: “Chuo kinafanya kila kiwezalo kuhakikisha mitihani inafanywa katika mazingira mazuri bila usumbufu wowote”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: