Kupandikiza mishipa mitatu ya damu katika moyo wa mgonjwa mwenye umri wa miaka arubaini

Maoni katika picha
Kikosi cha madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimefanikiwa kupandikiza mishiba ya damu mitatu katika moyo wa mgonjwa mwenye umri wa miaka (40), pamoja na kusafisha mishipa ya shingo ya upande wa kushoto.

Wakasema: “Mgonjwa alikua na tatizo la ubongo na kifua” akabainisha kuwa: “Baada ya kufanyiwa vipimo akagundulika kuwa na tatizo la kuziba mishipa ya damu ya kwenye moyo”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel daima hutoa huduma bora za matibabu kwa kutumia vifaa tiba vya kisasa ilivyo navyo, chini ya madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limeiwezesha kutoa ushindani mkubwa kwa hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali kila wakati, sambamba na kupokea wagonjwa waliopo katika hali tofauti za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: