Ripoti kuhusu ziara ya familia za mashahidi wa hospitali ya Imamu Husseini (a.s) katika mji wa Dhiqaar

Maoni katika picha
Ujumbe kutoka Ataba mbili takatifu Husseiniyya na Abbasiyya umetembelea wahanga wa ajali ya moto katika mkoa wa Dhiqaar kwenye hospitali ya Husseini (a.s) katika mji wa Naswiriyya kuwapa pole wafiwa na majeruhi wa tukio hilo.

Muwakilishi wa Atabatu Abbasiyya katika ujumbe huo na makamo rais wa kitengo cha Dini Shekh Aadil Wakili amesema kuwa: “Tulipokea hapari ya moto katika mkoa wa Dhiqaar kwenye kituo cha kuhudumia watu walioambukizwa virusi vya Korona katika hospitali ya Husseini (a.s) kwa majonzi na huzuni kubwa, katika ziara hii tumetembelea familia za wahanga na kuwafikishia salamu na rambirambi kutoka kwa watumishi wa malalo mbili tukufu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), zikiongozwa na viongozi wakuu wa kisheria katika Ataba hizo, na kumuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awarehemu ndugu zao na kuwaweka mahala pema peponi sambamba na kuwapa Subira na uvumilivu wafiwa, aidha tunaunga mkono uchunguzi unaoendelea na pindi wahusika walio sababisha moto huo watakapo bainika hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao”.

Kumbuka kuwa Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya husimama pamoja na raia wote wa Iraq, na hutoa misaada mbalimbali ya kibinaadamu kwenye majanga tofauti, likiwemo janga hili lililopoteza roho nyingi za watu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: