Muonekano wa furaha ya Ghadiir umetanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Mazingira ya shangwe na furaha yametanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kusherehekea sikukuu kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, Idul-Ghadiir. Ambayo kumbukumbu yake inasadifu siku ya Alkhamisi mwezi (18 Dhulhijjah).

Kuta zake zimepambwa mabango yaliyo andikwa maneno ya utii wa kudumu kwa kiongozi wa waumini Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s), mabango hayo ni kielelezo cha furaha kubwa waliyonayo wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika kuadhimisha kutangazwa kiongozi wa waumini na khalifa wa Mtume (s.a.w.w).

Kama kawaida yake katika kuadhimisha matukio ya furaha kwa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s), Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalum ya kuadhimisha tukio hili adhimu inayo endana na mazingira ya sasa.

Kumbuka kuwa siku ya mwezi kumi na nane Dhulhijjah mwaka wa kumi hijiriyya alitangazwa Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s) kuwa kiongozi wa waumini na khalifa wa Mtume (s.a.w.w).

Hivyo siku hiyo ni sikukuu tukufu mbele ya Mwenyezi Mungu na familia ya Mtume (a.s), Mwenyezi Mungu hakuwahi kutuma Nabii yeyote ispokua aliitukuza siku hiyo tukufu, siku hiyo mbingini inaitwa (siku ya ahadi iliyoahidiwa) na hapa ardhini inaitwa (siku ya ahadi iliyowekwa na kundi lililoshuhudia).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: