Baada ya kutengenezwa katika kiwanda cha Saqaa.. tunaadhimisha mwaka wa tatu tangu kuzinduliwa katika Atabatu Kadhimiyya tukufu dirisha mbili za kaburi zake

Maoni katika picha
Siku kama hizi miaka mitatu iliyo pita wakati wa kusherehekea Idul-Ghadiir, zilizinduliwa dirisha mbili mpya za kaburi la Shekhe Mufid na ustadh wake Ibun Qulawaihi Pamoja na Khawaja wa Nasru-Dini Tusi, uzinduzi huo ulifanywa ndani ya Atabatu Kadhimiyya Jirani na malalo ya Maimamu wawili -Alkadhimaini- (a.s), baada ya kutengenezwa katika kiwanda cha Saqaa kinacho husika na utengenezaji wa madirisha na milango ya makaburi na mazaru tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya takatifu.

Ilifanywa hafla kubwa ndani ya haram ya Maimamu wawili Alkadhimaini (a.s), iliyo hudhuriwa na wajumbe wa kamati kuu na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Muhammad Ashiqar, na muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu katika mji wa Kadhimiyya Shekh Hussein Aali Yaasin, bamoja na wawakilishi wa Ataba na mazaru tukufu na viongozi wa Dini, jamii na serikali, Pamoja na watumishi wa Ataba tukufu na mazuwaru, wakati wa kusherehekea Idul-Ghadiir ndani ya haram takatifu ya Kadhimiyya.

Madirisha hayo matukufu yalitengenezwa katika kiwanda cha Saqaa kwa umaridadi mkubwa na kuwekwa nakshi nzuri za kiislamu zinazo endana na utukufu wa eneo hili.

Hafla ya uzinguzi ilikua na vipengele vingi, ikiwa ni pamoja na mawaidha, kaswida na mashairi, yaliyo amsha hisia za furaha katika nafsi za waumini na mazuwaru watukufu, ikahitimishwa kwa shughuli ya kukabidhi funguo za madirisha hayo kutoka kwa katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Muhammad Ashiqar, ambaye alimkabidhi katibu mkuu wa Atabatu Kadhimiyya dokta Jamali Abdu-Rasuul Dabaaqh.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: