Mwezi ishirini na mbili Dhulhijjah aliuawa kishahidi Maitham bun Yahya Tammaar

Maoni katika picha
Mwezi ishirini na mbili Dhulhijjah aliuawa kishahidi Maitham Tammaar Asadiy Alkufiy (r.a) mwaka wa (60) hijiriyya, alikuwa katika wafuasi wa kiongozi wa waumini Ali (a.s) na msiri wake, pia alikua katika wafuasi wa Imamu Hassan na Hussein (a.s), kwa sababu alikua anauza tende katika mji wa Kufa akapewa jina la (Tammaar).

Alikua na elimu ya Munaya, Balaya na tafsiri, mwenye Imani kubwa na yakini, alikua na zuhudi mwenye kufunga mchana na kusimama usiku, mfasaha, mtendaji wa haki, alikua na heshima kubwa mbele ya Mtume (s.a.w.w), hadhi yake ilikua sawa na Salmaan mbele ya Mtume (s.a.w.w), alimuacha huru na kumuweka karibu yake, Ibun Ziyadi alimuuwa kwa sababu ya umashuhuri aliokua nao.

Maitham (r.a) alikua anatangaza utukufu wa Imamu Ali (a.s) na Ahlulbait kwa ujumla, na kutaja aibu za bani Umayya, hasa Muawiya na waliofuata nyayo zake, akaendelea kua anaeleza fadhila za bani Hashim.

Ibun Ziyadi alimwita akamuambia: Jitenge na Ali (a.s) na ueleze utukufu wa utawala wa Othumani au nitakata mikono yako na miguu yako na kukusulubu. Maitham (r.a) alikataa, akaendelea kutaja utukufu wa Imamu Ali (a.s), Ubaidu-Llahi bun Ziyadi (laana iwe juu yake) akaamuru akatwe mikono na miguu halafu asulubiwe kwenye ubao.

Alipo pandishwa juu ya ubao akaita kwa sauti ya juu akasema: Enyi watu, nani anataka kusikia hadithi kutoka kwa Ali bun Abu Twalib kabla sijauawa, wallahi nitakuambieni fitna zitakazo tokea hadi siku ya kiyama.

Watu wakamzunguka na akaanza kuwahadithia utukufu wa Ali bun Abu Twalib (a.s) na bani Hashim pamoja na maajabu yao, na maovu ya bani Umayya huku akiwa anateswa juu ya ubao.

Ubun Ziyadi akaambiwa: Amekufedhehesha huyu mtumwa, akasema: mpigeni mawe, wakampiga mawe baada ya kuwa ameshachoshwa na mateso, alikua mtu wa kwanza kupigwa mawe katika uislamu, baada ya uso na mdomo wake kujaa damu, ibun Ziyadi akaamuru akatwe ulimi, wakakata ulimi wake, ndevu zake zote zikalowa damu, kisha akachomwa mikuki ya kiunoni, akabiga takbira na roho yake takatifu ikatoka.

Ilipofika siku ya pili ya kusulubiwa kwake ndio alikatwa ulimi na siku ya tatu alichomwa mikuki na kuuwawa kishahidi, aliuwawa siku kumi kabla ya Imamu Hussein (a.s) kufika Iraq.

Alizikwa katika mji wa Kufa, kaburi lake lipo hadi leo watu huenda kulitembelea, lipo karibu na masjid Kufa upande wa kusini magharibi, kushoto kama ukiwa unaenda Kufa kutoka Najafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: