Mwezi ishirini na tatu Dhulhijjah kumbukumbu ya kifo cha Watoto wa Muslim bun Aqiil (a.s)

Maoni katika picha
Watoto wa Muslim bun Aqiil (a.s) ni kama baba yao, walionyesha ujasiri mkubwa mbele ya Imamu Hussein (a.s), wakafanya juhudi za kumnusuru mbele ya madhalimu, jambo hili sio geni kwani wao wanatokana na kizazi kitakatifu, kuuwawa kwao ni kawaida na utukufu wao mbele ya Mwenyezi Mungu ni shahada.

Muhammad na Ibrahim ni watoto wa balozi wa Hussein, Muslim bun Aqiil bun Abu Twalib (a.s), Watoto hao walishiriki katika vita tukufu ya Twafu, hakika tukio lao halikuchukua masiku au masaa bali lilidumu kwa muda wa mwaka mzima, mwezi ishirini na tatu Dhulhijjah ni siku ya kukumbuka kifo chao, ambacho kinaweza kuchukua nafasi ya pili kwa namna walivyo nyanyaswa na kudhulumiwa, baada ya kifo cha Imamu Hussein na dhugu zake na wafuasi wake Karbala.

Kwa mujibu wa historia Muhammad na Ibrahim walikua Pamoja na Imamu Hussein (a.s) katika ardhi ya Karbala, wakakimbia kutoka katika watu waliobaki wa familia ya Imamu, wakakamatwa na wanajeshi wa ibun Ziyadi na kuwa mateka kwa muda unaokaribia mwaka.

Baada ya kukimbia jela, walikamatwa na muovu mmoja aliyerubuniwa kupewa mali, akawapeleka pembeni ya mto wa Furaat, walipotambua kuwa anataka kuwaua, walisema: Ewe mzee..! katuuze sokoni utanufaika na pesa, yaani kama lengo lake ni kupata hela kwa ibun Ziyad, akiwauza atafikia lengo lake la kupata pesa, lakini yeye alisisitiza azma yake ya kuwaua, japokua walimjulisha kuwa wao ni miongoni mwa watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w).

Aliwaambia: ninakuuweni na kwenda kuchukua malipo kwa vichwa vyenu, kisha wakamuambia: Tupeleke kwa ibun Ziyadi tukiwa hai akatuhukumu yeye mwenyewe, yule mtu akakataa ombi hilo pia, akawaua pembezoni ya mto Furaat, akakata vichwa vyao na miili yao akaitupa kwenye maji ya mto Furaat.

Riwaya zinasema kuwa mtu huyo muovu alianza kumuua mtoto mkubwa, damu zikamrukia mtoto mdogo akasema: nitakutana na babu yangu Mtume wa Mwenyezi Mungu nikiwa nimeloa damu ya kaka yangu, kisha akamuua mtoto mdogo na kukata vichwa vyao, halafu miili yaoa akaitupa kwenye mto wa Furaat, akachukua vichwa vyao na kuvipeleka kwa ibun Ziyaad, halafu akamhadithia namna alivyo wakamata na kuwaua pamoja na majibizano yao, akakasirika akamnyima malipo na akaamuru auwawe.

Makaburi ya Watoto hao yapo umbali wa kilometa thelathini mashariki ya wilaya ya Musayyib, iliyopo upande wa mashariki ya mto wa Furaat, ambapo hivi sasa sehemu hiyo iko chini ya mji wa Hilla katikati ya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: