Kitengo cha maadhimisho na mawakibu: kimeanza mchakato wa kuratibu na kuwasiliana na mawakibu za Ashura

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimeanza kuratibu na kuwasiliana na mawakibu za Karbala, zitakazo shiriki katika kuomboleza na kutoa huduma wakati wa siku za Ashura.

Miongoni mwa maandalizi hayo ni kutoa vitambulisho na miongozo kwa viongozi wa mawakibu, ukizingatia kuwa wao ndio mamlaka ya kisheria pekee inayo wajibika kusimamia mawakibu kwa kushirikiana na vikosi vya usalama vya Karbala.

Rais wa kitengo hicho bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Utoaji wa vitambulisho na miongozo ni moja ya maandalizi muhimu, kwa lengo la kuratibu utendaji wa mawakibi na kulinda usalama wao kwa kushirikiana na vikosi vya usalama vya Karbala”.

Akaongeza kuwa: “Kazi yetu imegawanyika sehemu mbili, kwanza uratibu ambao ni jukumu maalum la kitengo chetu, na ulinzi ambao ni jukumu la vikosi vya usalama vya Karbala, katika utekelezaji wa majukumu hayo hutolewa vitambulisho kwa viongozi wa mawakibu, hairuhusiwi maukibu yeyote kutoa huduma bila kuwa na kitambulisho, hususan zitakazo omboleza au kutoa huduma ndani ya eneo la mji wa Karbala au kwenye miji na njia zinazo elekea Karbala”.

Kumbuka kuwa kitengo cha maadhimisho ndio mamlaka pekee inayo husika na kuratibu mawakibu na vikundi vya Husseiniyya, kutoa vitambulisho na maelekezo kwa kushirikiana na vikosi vya ulinzi na usalama vya Karbala, taasisi za kijamii ambazo hutoa huduma kwa mawakibu na vikundi vya Husseiniyya ni wasaidizi tu haziwajibiki kisheria.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: