Mawakibu za Karbala zinajiandaa kupokea mwezi mtukufu wa Muharam

Maoni katika picha
Watu wa Karbala mji mkuu wa maadhimisho ya Husseiniyya na mawakibu zao wameanza kufanya maandalizi ya kupokea mwezi wa huzuni ya kifo cha Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake (a.s) na wafuasi wake, msimu wa huzuni unasogea kidogo kidogo.

Kama ilivyo kawaida maandalizi huanza baada ya Idul-Ghadiir na huendelea hadi siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Muharam, rangi nyeusi imeanza kuenea katika mji huo wa shahada, mawakibu na vikundi vya Husseiniyya vinaandaa sehemu zao.

Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Watu wa Karbala walianza kufanya maandalizi ya kupokea mwezi mtukufu wa Muharam tangu siku saba zilizo pita, wamefanya maandalizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati ya ulinzi wa amani na utoaji wa huduma za afya”.

Akaongeza kuwa: “Huu ni mwaka wa pili tunaishi katika mazingira magumu kiafya, kutokana na kuwepo kwa maambukizi ya virusi vya Korona, mwaka huu umekua na maandalizi ya pekee kutokana na kuwepo kwa janga hilo”.

Akamaliza kwa kusema: “Maandalizi hayo yalitanguliwa na vikao kati ya viongozi wa mawakibu na wawakilishi wa vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na taasisi za kiserikali, katika vikao hivyo tulikubaliana vitu vingi vinavyo lenga kufanikisha maombolezo hayo na kutoa picha halisi ya mapinduzi ya Imamu Hussein (a.s)”.

Kumbuka kuwa barabara na chochoro za mji wa Karbala na sehemu inayo zunguka eneo ya malalo mawiti matakatifu, inashuhudiwa kazi ya ujenzi wa mabanda na mahema ya kutolea huduma mbalimbali kila siku, huo ni utamaduni mkubwa wa watu wa Karbala wakati wa maombolezo, jambo hilo ni urithi kutoka vizazi na vizazi vya watu wa mji huo mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: