Kuanza kutoa chanjo ya Korona kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya watukufu

Maoni katika picha
Idara ya Swidiiqatu-Twahirah (a.s) ya madaktari wa kike, imeanza kutoa chanjo ya Korona kwa watumishi wa kike katika Atabatu Abbasiyya tukufu na familia zao pamoja na wanafunzi wa shule za wasichana za kidini, kwa lengo la kupunguza maambukizi ya virusi hivyo wakati wa ziara.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa Idara bibi Bushra Kinani, amesema: “Zoezi la utoaji wa chanjo linafanywa kwa kushirikiana na hospitali ya rufaa Alkafeel na idara ya madaktari pamoja na shule za kidini Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya, itatolewa kwa watumishi wote pamoja na familia zao kama ilivyo pangwa, nayo ni sehemu ya mkakati wa Atabatu Abbasiyya wa kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona”.

Akasisitiza kuwa: “Chanjo imekua jambo muhimu kutokana na kuongezeka kwa maambukizi, kwani inasaidia kupunguza uwezekano wa kuambukizwa, na kulinda afya ya muili sambamba na kulinda usalama wa watu wengine”.

Akafafanua kuwa: “Chanjo imepatikana baada ya kuwasiliana na idara ya afya ya mkoa wa Karbala, kuna jopo maalum la wataalamu kwa ajili ya kutoa chanjo hiyo, pamoja na kuandaa mahitaji yote, utoaji chanjo utafanywa kila siku hadi watumishi wa kike wote katika Atabatu Abbasiyya tukufu watakapo maliza kuchanjwa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: