Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu amekutana na marais wa vitengo na wasaidizi wao

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya asubuhi ya Jumamosi ya mwezi (27 Dhulhijjah 1442h) sawa na tarehe (7 Agosti 2021m), umefanya kikao kikubwa kilicho ongozwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi cha kujadili mambo mbalimbali yanayo husu utoaji wa huduma kwa mazuwaru.

Katika kikao hicho alikuwepo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Muhammad Ashiqar na naibu wake Mhandisi Abbasi Mussawi Ahmadi pamoja na wajumbe wa kamati kuu.

Wamejadili mambo mengi yanayo husu utoaji wa huduma kwa mazuwaru, vitengo vinavyo husika vimehimizwa kuhakikisha vinaboresha huduma zao kwa wageni watakaokuja katika malalo hii takatifu.

Hali kadhalika wamejadili maandalizi ya kupokea mwezi wa Muharam na Safar pamoja na kuweka mpango kazi wa vitengo na idara tofauti, hususan katika sekta ya usalama na afya, ili kuhakikisha wageni wanafanya ziara kwa amani na utulivu.

Sayyid Swafi amepongeza kazi zinazo fanywa na watumishi wa malalo hii takatifu, aidha amepongeza miradi ya ujenzi iliyokamilika hivi karibuni, akahimiza kuendelea kutoa huduma bora kwa mazuwaru watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: