Kupokea bendera za uombolezaji wa Husseiniyya kwa wawakilishi wa mawakibu mikoani

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimepokea bendera za kuomboleza msiba wa Imamu Hussein (a.s) kupitia wawakilishi wake waliopo katika mikoa tofauti ya Iraq, zitakazo pandishwa katika usiku wa kwanza wa mwezi wa Muharam, kupandishwa bendera hizo huwa sawa na tangazo la kuanza maombolezo ya Ashura, huenda sambamba na shughuli ya kubadilisha bendera ya kubba la malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Rais wa kitengo hicho bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Wawakilishi wa kitengo katika kila usiku wa kwanza wa mwezi wa Muharam hupandisha bendera zinazo ashiria kuanza msimu wa huzuni za Aali Muhammad (s.a.w.w), na kukumbuka kifo cha baba wa watu huru Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake (r.a), kitendo hicho hufanywa na wawakilishi wa kitengo cha maadhimisho katika mikoa yote ya Iraq”.

Akaongeza kuwa: “Kila mkoa unasehemu maalum ya kupandishia bendera, kila upande wa bendera umeandikwa (Yaa Hussein) na (Yaa Qamaru bani Hashim), huwa kuna shughuli ndogo ya uombolezaji wakati wa kupandisha bendera hizo, zinazo ashiria maneno ya bibi Zainabu (a.s), alipo sema kuwa haki itabaki juu daima, na itapepea juu ya vichwa, tena itakua taa linaloangazia misingi ya mapinduzi ya Imamu Hussein (a.s)”.

Tambua kuwa upandishaji wa bendera za huzuni umekua utamaduni wa maadhimisho ya Husseiniyya, waumini wamezowea kufanya hivyo ndani na nje ya Iraq, kama tangazo la kuanza msimu wa huzuni za kuuwawa kwa Imamu Hussein (a.s) na kuingia mwezi mtukufu wa Muharam.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: