Twende kwenye msiba: Kubadilisha bendera ya kubba la Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Baada ya swala ya Isha leo mwezi (29 Dhulhijjah 1442h) sawa na tarehe (9 Agosti 2021m), bendera za kubba mbili ya haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), zimebadilishwa bendera nyekundu na kupandishwa nyeusi, kama ishara ya kuanza msimu wa huzuni za Ashura, ambazo siku yake ya kwanza itakuwa kesho Jumanne kwa mujibu wa kuandama kwa mwezi wa Muharam (1443h) chini ya taarifa ya ofisi ya Mheshimiwa Sayyid Sistani.

Bendera zimebadilishwa bila hafla yeyote wala kukusanyika watu wengi kwa mwaka wa pili mfululizo kutokana na mazingira ya kiafya yaliyopo hapa Iraq na duniani kwa ujumla.

Kumbuka kuwa Ataba mbili tukufu zilikua zimesha tangazo kutokuwepo kwa hafla wakati wa kubadilisha bendera ya kubba la malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya mazingira ya afya na kulinda usalama wa mazuwaru.

Bendera nyekundu inamaanisha kuwa mwenye kaburi husika aliuwawa na bado kisasi chake hakijalipizwa kwa mujibu wa desturi za waarabu, na bendera nyeusi inamaanisha msiba na huzuni, kila mwaka huwa tunabadilisha bendera kwa kushusha nyekundu na kupandisha nyeusi ambayo hubaki hadi mwanzoni mwa mwezi wa Rabiul-Awwal, ndipo hutolewa na kurudishwa nyekundu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: