Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa pole kwa mkurugenzi wa mji wa Karbala

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu unatuma salam za rambirambi na kutoa pole kwa mkurugenzi wa mji wa Karbala, kufuatia kifo cha mhandisi Ustadh Abiir Salim Naaswir Alkhafaji aliyefariki wakati akitekeleza majukumu yake.

Wakati huohuo Ataba inatoa pole kwa watu wa Karbala kutokana na msiba huo, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu, amuweke mahala pema peponi pamoja na waja wake wenye ikhlasi, ampokelee huduma alizotoa kwa watu wake.

Ewe Mola muweke mahala pema katika akhera yako, kama ulivyo mtoa duniani akiwa mahala pema.

Ewe Mola mpe matarajio yake, na umkutanishe na Muhammad na Aali Muhammad, umuweke katika pepo ya Firdaus.

Ewe Mola ipe Subira na uvumilivu familia yake na marafiki wake, hakika sote ni amana.

Hakika sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea..
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: