Ibun Ziyaad awatisha watu wa Kufa na awakataza wasimsaidie Imamu Hussein (a.s)

Maoni katika picha
Kufuatia kukatazwa watu wa Kufa wasimsaidie Imamu Hussein (a.s) na kuwatisha, Ubaidullah bun Ziyaad kiongozi wa Kufa siku ya nne katika mwezi wa Muharam mwaka wa 61 hijiriyya, alitoa khutuba kali na kumtisha kila atakae jaribu kumsaidia Imamu Hussein (a.s) atateswa na kuuawa, katika khutuba hiyo akasoma fatwa ya Shuraihi Qadhi iliyo halalosha damu ya Imamu Hussein (a.s), akaamuru barabara zote zinazo ingia katika mji wa Kufa zifungwe.

Riwaya zinaonyesha kuwa vitisho na mateso ndio mbinu aliyotumia ibun Ziyaad, watu wenye nafsi dhaifu akawavutia kwa kuongeza malipo yao na viongozi wa makabila na wenye madaraka akawapa mali zaidi, waliokua na msimamo aliwakamata na kuwatia jela, wengi wao baada ya kutoka jela walifanya harakati za watubiao chini ya uongozi wa Suleiman bun Swardi Alkhuzai na wafuasi wake.

Amma viongozi wa makabila waliompinga aliwakamata akawatesa na kuwafunga, tunatambua anaeshawishi watu katika muelekeo sahihi, watu humsikiliza na kumtii, viongozi wa makabila ya kufa walikua wamegawanyika kikabila, walikuwepo Umawiyyiin na Alawiyyiin, ibun Ziyaad akawatumia Umawiyyiin kuwashambulia Alawiyyiin walio mkhalifu.

Makabila yakapoteza viongozi wao na yakasambaratika kutokana na khofu iliyojengwa na ibun Ziyaad, vitisho na mateso, alisambaza majasusi kila sehemu na akaweka walinzi kwenye njia zote zinazo ingia katika mji wa Kufa, akawaambia kuna jeshi kubwa linakuja kutoka Sham, katika mazingira hayo mtu dhaifu aliyekosa mawasiliano na kiongozi wake hawezi kupambana.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: