Kukamilika idadi ya wanajeshi walikwenda kupigana na Imamu Hussein (a.s), na Ahlulbait na wafuasi wa Imamu (a.s) wanazidi kuwa na msimamo

Maoni katika picha
Kwa mujibu wa riwaya za kihistoria wanajeshi waliokuja kutoka Sham kwa ajili ya kupigana na Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake, chini ya uongozi wa Omari bun Saadi, idadi yao ilifika elfu (40) katika siku ya tano ya mwezi wa Muharam mwaka wa 61h.

Upande wa pili watu wa nyumba ya Imamu Hussein (a.s) na wafuasi wake waliendelea kuwa na msimamo imara wa kumnusuru Imamu hadi done la mwisho la damu yao, wala hawakuhofishwa na wingi wa maadui waliowazunguka, bali uliwazidishia imani na msimamo wa kumnusuru Imamu Hussein (a.s), hakika walikua kama alivyo sema yeye mwenyewe (a.s): (Hakika mimi sijui wafuasi waaminifu na bora kushinda wafuasi wangu, wala watu wa nyumbani wenye mshikamano zaidi kushinda watu wa nyumba yangu, Mwenyezi Mungu akulipeni kheri).

Jeshi la ibun Ziyaad liliimarisha ulinzi katika mji wa Kufa, na kuzuwia wakazi wa mji huo wasiende kumnusuru Imamu Hussein (a.s).

Watu waliendelea kutumwa katika mitaa ya mji wa Kufa kuhimiza watu watii utawala wa ibun Ziyaad na kuwajengea hofu, kuwa atapata mwisho mbaya yeyote atakae asi utawala huo, na kuwataka waungane na jeshi la Yazidi.

Ibun Ziyaad aliendelea kutuma askari kwa ibun Saadi hadi wakatimia elfu thelathini, na yeye akaongoza jeshi, baadhi ya riwaya zinathibitisha kua jeshi lililo pigana na Imamu Hussein lilikua na wapiganaji elfu thelathini, ibin Ziyaad akaweka walinzi katika milima ya mji wa Kufa, ili asitokee yeyote wa kwenda kumsaidia Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: