Siku ya saba ya Muharam na kuhusishwa kwake na Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Siku ya saba ya mwezi mtukufu wa Muharam husasibishwa na Abulfadhil Abbasi (a.s), riwaya zinaonyesha kuwa, katika siku hiyo mwaka wa (61) hijiriyya, Imamu Hussein (a.s) na watu wake, waliishiwa maji waliyokua nayo, maadui wakaimarisha ulinzi katika njia ya kwenda mtoni kuchota maji.

Imamu Hussein (a.s) na watu wake wakazidiwa na kiu, kama kawaida watoto wakawa wanalia kwa kiu ya maji, yote hayo yanatokea mbele ya Abu Abdillahi Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake watukufu, upatikanaji wa maji ulikua mgumu kwao, kwani jeshi la maadui lilikua limesimama imara kuwazuwia kuchota maji likiwa na mikuku, mishale na mapanga makali, lakini myweshaji wenye kiu hakuweza kuvumilia hali hiyo. Alimuomba ruhusa ndugu yake ya kwenda kuchota maji, Imamu (a.s) akamruhusu, akampa watu ishirini wakiwa na viriba vya kuchotea maji, wakaondoka na kuelekea mto wa Furaat usiku bila kuogopa wanajeshi waliozingira mto huo, kwani wako pamoja na simba wa Aali Muhammad, mtoto wa Karaar Abulfadhil Abbasi (a.s), akatangulia Naafiy bun Hilali Aljamaliy akiwa amebeba bendera, Omari bun Hajjaaj akasema: Nani wewe na unataka nini? Naafiy akasema: Nimekuja kunywa maji mnayo tuzuwia. Akasema: Kunywa na usibebe hata kidogo kumpelekea Hussein.

Naafiy akasema: Hapana, Wallahi siwezi kunywa hata tone la maji wakati Hussein na watu alionao wanakiu. Naafiy akawaambia watu wake, jazeni viriba vyenu. Wanajeshi wanao ongozwa na ibun Hajjaaji wakawavamia, wakawa baadhi wanachota maji na wengine wanapigana chini ya jemedari Abulfadhil Abbasi (a.s).

Wakachota maji na wakafanikiwa kuyafikisha hadi kwenye mahema, wakapoza kiu watu wa Imamu Hussein pamoja na watoto.

Tukio hilo lilijirudia tena siku ya mwezi kumi Muharam, alipo pigana na askari waliokua wanalinda mto hadi akawashinda, akafika mtoni na akachota maji, lakini wakati anarudi, maadui walimvamia kwa wingi na wakafanikiwa kutoboa kiriba cha maji katika mapambano makali, nguvu zikamuisha na maadui wakamzunguka kila upande wakamshambulia vikali mno hadi akafa kishahidi (amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: