Kitengo cha mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu: Uhusiano wake na mawakibu Husseiniyya za kutoa huduma

Maoni katika picha
Uhusiano kati ya mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu na mawakibu Husseiniyya zinazo toa huduma umeanza zamani, mwaka baada ya mwaka uhusiano huo unaongezeka, kinacho tuunganisha ni kuwahudumia mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Rais wa kitengo Mhandisi Aadil Hamaami ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Uhusiano kati ya Atabatu Abbasiyya tukufu na mawakibu Husseiniyya za kutoa huduma umeanza muda mrefu, mwaka baada ya mwaka uhusiano huo unaongezeka, kinacho tuunganisha ni utoaji wa huduma kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaongeza kuwa: “Uhusiano wetu upo katika mambo mengi, ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wakati wa msimu wa ziara, ikiwemo ziara ya mwezi kumi Muharam, ambayo huwa ni maalum kwa watu wa Karbala takatifu na mawakibu zao”.

Akafafanua kuwa: “Mgahawa umetoa misaada tofauti kwa mawakibu hizo, kama vile chakula, maji na vitu vingine walivyo hitaji, hutoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru katika siku ya kumi Muharam, kutokana na wahudumu wengi wa mawakibu kushughulishwa na uombolezaji”.

Akamaliza kwa kusema: “Hakika mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu ni nguzo muhimu kwenye utoaji wa huduma katika mji huu mtakatifu, ambao kuhudumia mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) ndio utukufu wake”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: