Undugu, uaminifu, ushujaa na kujitolea.. miongoni mwa sifa za Abulfadhil Abbasi (a.s) zinazo tajwa na mawakibu za waombolezaji katika malalo yake

Maoni katika picha
Siku kumi za kwanza katika mwezi mtukufu wa Muharam, zimegawanywa kwa watu waliokuwa na Imamu Hussein (a.s) katika jangwa la Karbala, historia imeandikwa kwa herufi za nuru, walipata utukufu mkubwa wa milele na milele, hakika nafsi zao zimetakasika na majina yao yanatajwa kizazi hadi kizazi.

Miongoni mwa siku zenye athari kubwa ni siku ya mwezi saba Muharam, kwa nini isiwe hivyo nayo ni siku inayonasibishwa na Abulfadhil Abbasi (a.s), maukibu zote zinazo kuja kufanya ziara na kuomboleza katika malalo mbili takatifu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) zinataja msimamo na ushujaa wake.

Kwa namna alivyo simama imara na ndugu yake Abu Abdillahi Hussein (a.s), na nafasi yake katika uwanja wa vita ya Karbala, katika kulinda famila ya Mtume (s.a.w.w), hadi mmoja wa viongozi wa jeshi la ibun Ziyaad akasema: Hakika nguvu ya jeshi la Hussein (a.s) ipo katika upanga wa Abbasi (a.s), maadui hawakuweza kushinda jeshi la Imamu Hussein (a.s) hadi walipo muua na kukata mikono yake wakati anakaribia kupata shahada (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: