Zaidi ya mita 5000 za kapeti zimetandikwa katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imetandikwa kapeti lekundu lenye ukubwa wa zaidi ya mita za mraba (5000), kazi hiyo imefanywa na watumishi wa kitengo cha usimamizi wa haram takatifu wakati wa maandalizi ya kupokea mazuwaru na mawakibu za uombolezaji.

Makamo rais wa kitengo hicho Ustadh Zainul-Aabidina Quraishi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kutandika makapeti ndani ya haram ni moja ya kazi yetu, huwa tunafanya hivyo kila wakati wa kujiandaa na ziara ya Ashura, ili kuipa haram muonekano wa huzuni, na kuhakikisha matembezi yanafanyika vizuri bila msongamano”.

Akaongeza: “Makapeti tulilopewa na kitengo cha hazina katika Atabatu Abbasiyya tukufu, yametandikwa vizuri kwa namna ambayo hayajikunji wala kutanduka kirahisi, kwani tumeweka gundi, makapeti hayo yametandikwa sehemu zote za haram tukufu”.

Akafafanua: “Kabla ya kutandika makapeti tulianza kupiga deki katika haram tukufu na kupuliza dawa, kisha tukatandika nailoni kwa kiwango kilekile cha kapeti, kwa kuzingatia maelekezo ya idara ya afya ya Atabatu Abbasiyya, aidha utaratibu wa kupuliza dawa, kutumia vitakasa mikona na kuvaa barakoa unaendelea”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: