Vikao vya kuomboleza katika maeneo tofauti ya Nainawa kwenye kumbukumbu ya Ashura

Maoni katika picha
Kamati ya msaada na maelekezo chini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya majlisi katika maeneo tofauti ya mkoa wa Nainawa.

Miongoni mwa maeneo hayo ni: Bartwala, Bazuya, Karmalisi na Khazana, mihadhara mbalimbali imetolewa na kaswida za huzuni zilizo amsha hisia za majonzi ya kifo cha bwana wa mashahidi (a.s), idadi kubwa ya wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wanaoishi kwenye miji hiyo wameshiriki katika majlisi hizo.

Majlisi zimesimamiwa na kamati tajwa wakati wa msimu huu wa huzuni za Husseiniyya katika mkoa wa Nainawa.

Kumbuka kuwa wapenzi wa Ahlulbait (a.s) katika vitongoji tofauti vya mkoa wa Nainawa, wanaomboleza kifo cha Imamu Hussein (a.s) kilicho tokea Karbala mwaka 61 hijiriyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: