Muhimu (kwa picha).. kuanza matembezi ya towareji

Maoni katika picha
Baada ya swala ya Adhuhuri siku ya Alkhamisi, mwezi kumi Muharam mwaka (1443h) sawa na tarehe (19 Agosti 2021m) matembezi ya uombolezaji ya Towareji yameanza.

Matembezi yameanzia katika kituo cha Salam yanapitia barabara ya Jamhuriyya, hadi katika Atabatu Husseiniyya tukufu halafu yatapita katika uwanja wa katikati ya haram mbili na kumalizia kwa kuingia katika Atabatu Abbasiyya.

Ulinzi umeimarishwa na kanuni za afya zimezingatiwa katika maeneo yote tuliyotaja, watoa huduma wa Ataba mbili wamejipanga vizuri kuhakikisha maombolezo haya yanafanywa kwa amani na utulivu.

Matembezi ya Towareji ni utamaduni uliozoweleka, yalianza kufanywa na watu wa Towareji (Wilaya ya Hindiyya iliyopo katika mkoa wa Karbala kilometa 20 kutoka makao makuu ya Karbala), kama ishara ya kuitikia wito wa Imamu Hussein (a.s) aliotoa siku ya mwezi kumi Muharam (Je kuna wa kunusuru aninusuru??), ni miongoni mwa matembezi yanayo husisha watu wengi zaidi duniani, yalianza mwaka (1303h) sawa na mwaka (1885m).

Ikumbukwe kuwa yalianza usiku wa mwezi kumi Muharam baada ya kumaliza majlisi ya kuomboleza katika nyumba ya Sayyid Swalehe Qazwini, lilitoka kundi la watu likiita (Waa Hussein.. waa Hussein) walizunguka katika mitaa ya mji huo, kisha miaka iliyofuata wakawa wanatembea hadi Karbala baada ya kuswali Adhuhuri katika kituo cha Salam, ambacho kipo umbali wa kilometa (5) kutoka lilipo kaburi la Imamu Hussein (a.s), matembezi hayo yakitanguliwa na kundi la watu wa Towareji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: